Agonga Nyumba ya Ex wake kwa Lori

Agonga Nyumba Ya Ex Wake Kwa Lori

 Hahahaha! Make hapa kwanza ncheke, ila jamani kuna watu wamevurugwa, basi bwana kutokea huko nchini marekani kijana mmoja kabomoa nyumba ya ex wake kwa kuigonga na lori.

Kijana huyo alietambulika kwa jina la Derek Wellington (34) wa Uingereza ametakiwa kulipa pound 475,000 (Bilioni 1.3 Tsh., Ksh. milioni 68) kama fidia baada ya kubomoa nyumba ya mpenzi wake wa zamani Sara Cassidy kwa kuigonga na lori kutokana na ugomvi wa kimapenzi uliokuwa ukiendelea baina yao.

Mahakama ilitoa amri ya kuachana kwao na ikamtaka Derek Wellington kutokumsogelea Sara lakini licha ya agizo hilo la Mahakama Derek aliendelea kumpigia simu Sara na kumwambia kuwa ipo siku ataendesha gari lake aina ya Lori na kuvunja nyumba yake ili akose mahali pa kulala, gazeti la The Sun limeripoti.

“Nitalipitisha lori langu hadi kwenye sebule yako” Derek alisikika akimwambia Sara kabla ya kutekeleza adhima yake hiyo.

 


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post