Afungwa kwa madai ya uongo ya kubakwa aliyoyatoa

Afungwa kwa madai ya uongo ya kubakwa aliyoyatoa

Mwanamke mmoja kutoka nchini Uigereza aliefahamika kwa jina la Eleanor Williams aliyetoa madai ya udanganyifu kwamba alibakwa na wanaume wengi na kusafirishwa kiharamu na genge la wanaume wanaopewa mafunzo Asia amefungwa gerezani miaka minane na nusu.

Mwanadada huyo ambae alisababisha maandamano katika mji Barrow nchini Uingereza anakoishi baada ya kutuma picha kwenye mitandao ya kijamii za majeraha ambayo alisema yalisababishwa na kipigo alichopata.

Mahakama ya Preston Crown Court ilibaini kuwa alijisababishia majeraha mwenyewe. Binti huyo mwenye miaka 22, alipatikana na hatia ya kupotosha njia ya haki.

Katika hukumu iliyosomwa kwa muda wa siku mbili, mahakama iliambiwa kuwa wanaume watatu ambao Eleanor aliwashutumu kwa uongo kwa kipindi cha miaka mitatu walijaribu kujiua baada ya shutuma hizo kutokana na kutengwa na watu.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags