Afunga ndoa ya siri baada ya mume wake kujiua

Afunga ndoa ya siri baada ya mume wake kujiua

Muigizaji kutoka nchini #Marekani, #AshleyJensen anadai kufunga ndoa kwa siri baada ya kufiwa na mume wake miaka sita iliyopita.

Ni miaka sita tangu nyota huyo wa ‘Shetland’ kumpoteza mume wake kwa kujiua, sasa ameamua kufunga ndoa ya siri na muigizaji mwenzie Kenny Doughty.

Kwa mujibu wa Gazeti la The Mail on Sunday limeeleza kuwa nyota huyo mwenye umri wa miaka 54, alifunga ndoa hiyo katika ukumbi wa kihistoria wa Priston Mill.

Mwigizaji huyo kwa sasa anaigiza katika tamthilia ya BBC Shetland, pia aliwahi kuigiza katika filamu ya ‘mahiri Rosie’ na nyengine nyingi.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post