Afunga ndoa na rice cooker

Afunga ndoa na rice cooker

Na Aisha Lungato

Eeeeeh bwana weeee waswahili wanasema ukistaajabu ya mussa utayaona ya filauni wewe ukiihangaika kutafta mahari kwenda kumuoa binti fulani wenzako wanafanya uamuzi konki sanaaa, Khoirul Anam ni mwanaume kutoka nchini Indonesia ambaye amefunga ndoa na rice cooker ili iwe mkewe.

Ndoa hiyo ilifungwa Septemba 20, 2021 ambapo bwana harusi huyo alivaa mavazi rasmi na kupewa cheti cha ndoa kwa kuoa chombo hicho cha umeme kinachotumika kupikia wali.

Rice cooker hiyo ilivalishwa mtandio katika siku hiyo muhimu kwa kwenda kuanza maisha mapya ya ndoa.

Khoirul Anam anasema yeye ni mweupe (fair), hapendi kuzungumza sana na pia anapenda kupika na amelipenda sana rice cooker hilo na kuamua kulioa kabisa liwe mke wake huku akilimwagia mabusu kama yote.

Baada ya ndoa hiyo iliyoowaacha watu midomo wazi, jamaa huyo alijitosa mitandaoni kuposti picha za siku yake hiyo muhimu kwa kufunga ndoa ingawa bado hajaposti picha za fungate (honeymoon) na mkewe huyo.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Saphinia Suleiman

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, career, skills development and technology.


Latest Post

Latest Tags