Afunga ndoa na mdoli

Afunga ndoa na mdoli

Mwanadada mmoja kutoka nchini Marekani aitwaye Felicity (24) anadaiwa kufunga ndoa na #mdoli aina ya #zombie aitwaye #Robert wiki moja iliyopita katika siku ya Wapendanao Febriari 14, 2024.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari nchini humo vinaeleza kuwa wawili hao walifahamiana miaka 7 iliyopita na kuchumbiana mwezi Novemba mwaka jana.

Ndoa hiyo ilihudhuriwa na watoto wao 10 ambao pia ni midoli, kufuatiwa na video zinazosambaa mitandaoni ambazo ziliwashangaza wengi baada ya mdoli huyo wakiume kumuuliza #Felicity kama amekubali kuolewa naye na kumvumilia katika shida na raha.

Hata hivyo katika moja ya mahojiano aliyoyafanya mwanadada #Felicity alieleza njia anazotumia kuwasiliana na #midoli hiyo ambapo aliweka wazi kuwa huwa anawasiliana nayo kupitia hisia, mawazo pamoja na ndoto.

Hii siyo mara ya kwanza kwa #Felicity kufunga ndao na mdoli mwaka 2018 aliwahi kufunga ndao na mdoli aitwaye #Kelly.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags