Afro king fasheni ya nywele inayobamba

Afro king fasheni ya nywele inayobamba

 

Ni siku nyingine tena tunakutaka ili kujuzana mambo mbalimbali kuhusiana na masuala ya urembo, mitindo na mavazi ambayo najua uwenda unayajua ila mimi nakujua zaidi.

Msomaji wetu leo tutaangalia aina ya nywele ijulikanayo Afro King jinsi ambavyo aipitwi na wakati na imekuwa ikipendwa na wanawake wengi hapa mjini.

Kwa wafuatiliaji wa mambo ya urembo na mitindo watakumbuka kuwa staili hii ya Afro King ni staili iliyotoka muda mrefu lakini kila mwaka inakuja kivingine na kuwafanya wanawake kuendelea kuipenda zaidi.

Nywele hii inasukwa na kila mtu yaani wanawake mastaa na wasio mastaa na miongoni mwa mastaa waliowahi kusuka nywele hizi ni pamoja na Jokate Mwigelo, Wema Sepetu kwa hapa nchini na kwa nje waliovutiwa na staili hii ni msanii Rihanna na Tyra Bank.

Afro King zinapatikana kwa rangi nyingi kama vile Bluu, Zambarau, pinki pamoja na rangi ya kahawia ‘brown’. Hata hivyo watu wengine utumia nywele hizo pia kuunganisha katika dredi zao.

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm


Latest Post

Latest Tags