Afghanistan, watu 10 wauawa katika shambulio la bomu shule ya kidini

Afghanistan, watu 10 wauawa katika shambulio la bomu shule ya kidini

Afisa wa Taliban amesema mlipuko wa bomu uliotokea katika shule ya kidini kaskazini mwa Afghanistan umesababisha vifo vya wanafunzi wasiopungua 10.

Mlipuko huo ulitokea wakati wa sala ya mchana katika Madrasa ya Al Jihadi mjini Aybak, ambao ndiyo mji mkuu wa mkoa wa Samangan. Kulingana na mkazi aliezungumza na shirika la habari la Associated Press, kwa sharti la kutotajwa jina, wanafunzi wengi walioko kwenye shule hiyo ni wavulana.

Picha za vidio zilizotolewa na vyombo vya habari zimeonesha eneo la mlipuko, ukumbi uliojaa vifusi, mikeka na viatu, kukiwa na maiti na damu iliyotapaa sakafuni.

Aidha msemaji wa wizara ya mambo ya ndani Abdul Nafi Takor, amesema wanfunzi kadhaa pia wamejeruhiwa katika shambulio hilo.

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags