Afariki kwa kugongwa na gari akiwasaidia bata kuvuka barabara

Afariki kwa kugongwa na gari akiwasaidia bata kuvuka barabara

Mwanamume mmoja kutoka nchini California aliefahamika kwa jina la Casey Rivara amefariki baada ya kugongwa na gari ambapo alionekana akisaidia bata kuvuka barabara muda mfupi kabla ya tukio hilo, polisi wa eneo hilo walisema.

Rivara alitoka kwa gari lake kabla ya kugongwa na dereva kijana huko Rocklin, karibu kilomita 40 kaskazini mashariki mwa Sacramento, polisi wa jiji walisema.

“Mwanamume huyo aliripotiwa kujaribu kusaidia watoto wa bata walioyokuwa kwenye barabara," Idara ya Polisi ya Rocklin ilisema katika taarifa.

Summer Peterson, mmoja wa mashuhuda aliambia mshirika wa karibu wa CBS News kwamba watoto wake walishuhudia ajali hiyo, ambayo ilitokea Alhamisi usiku mwendo wa saa mbili na robo usiku.

Watu wameweka maua na bata wa mpira katika eneo la ajali hiyo kwa heshima yake huku mpaka sasa hakuna mtu aliyekamatwa kuhusiana na tukio hilo.


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post