Adaiwa kuvunja rekodi kwa kupika masaa 227

Adaiwa kuvunja rekodi kwa kupika masaa 227

Mwanamke mmoja kutoka nchini Ghana aitwaye Chef Faila anadaiwa kuipiku na kuvunja rekodi ya Alan Fisher kwa kupika masaa 227.

Aidha mwanamke huyo anasubiri uthibitisho kutoka kwa ‘Guinness World Records’ ambapo kupitia ukurasa wa X wa kitabu hicho cha rekodi za dunia, wametolewa majibu ya kuwa wanapitia video za siku zote ili kuthibitisha hilo.

Iwapo Chef Faila atafanikiwa, atakuwa mtu wa kutoka Ghana kuingia kwenye kitabu hicho.

Ikumbukwe kuwa rekodi hiyo ilishikiriwa na Alan Fisher ambaye alipika kwa saa 119, dakika 57 na sekunde 16, rekodi hiyo ilithibitishwa mwezi Novemba mwaka 2023.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags