Abu Salami: Davido anaishi maisha ya uongo

Abu Salami: Davido anaishi maisha ya uongo

Mpiga ‘picha’ na mfanyabiashara #AbuSalami amedai kuwa msanii kutoka nchini #Nigeria #Davido hana pesa bali msanii huyo anaishi maisha ya uongo.

Hii inakuja baada ya mpiga ‘picha’ huyo kutoelewana na #Davido katika simu kuhusiana na deni la N218 Milion kwa ajili ya mradi wa watoto. Ambapo amedai kuwa msanii #BurnaBoy na #Rema ni matajiri kushinda #Davido.

Hii ni mara ya pili mwaka huu kwa Davido kushutumiwa kwa kushindwa kutimiza majukumu ya kimkataba, hapo awali, Rais wa zamani wa Shirikisho la ‘Soka’ la Nigeria, Amaju Pinnick, alimuita hadharani Davido kwa kutoheshimu mkataba wake nao.

Davido ambaye kwasasa anatamba na album yake ya ‘Timeless’ huku wimbo ambao umeibeba albamu hiyo ukiwa ni ‘Unavailable’.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags