Abaeme Onyenyi Arseface make-up artist kutoka Nigeria mwenye uwezo wa kubadilisha muonekano wa sura yako kuwa kama zombi

Abaeme Onyenyi Arseface make-up artist kutoka Nigeria mwenye uwezo wa kubadilisha muonekano wa sura yako kuwa kama zombi

Sehemu pekee unakupa burudani ni hapa Mwananchi Scoop, we outside the county yoooh this week tumetimba moja kwa moja hadi Nigeria, kukutana na Abaeme onyinye stellamaris Arseface Make-up Artist ( Film Make-up artist).

Usijali nipo kwa ajili yako najua utakuwa unajiuliza Arseface make-up ni kitu gani? acha nikusanue hizo ni make-up za kutisha zenye kubadilisha sura ya mtu na kuwa na muonekano mwingine , kama vile zombie movies ambazo huwa mnaziogopa zinaingia, pamoja na movie za kuonesha vidonda zote hizo ni Arseface make-up.

Kwenye safari yetu ya Nigeria mrembo Obaeme anatueleza she started her Arseface Make-up carrier mwaka 2018, akiwa hajui chochote kuhusu aina hizo za make-up. alikuwa akiangalia American Movie anajiuliza inakuwaje mtu anabadilishwa sura na kuwa anatisha na inakuwaje hadi mtu anaonekana kama anavidonda vya ukweli?.

Kuanzia hapo ndipo akaanza kutaka kujua namna ambavyo watu wanabadilishwa hadi kuwa na muonekano mwingine, wakati huo alikuwa akijua kupaka aina nyingine za make-up, kama vile beauty make-up, editorial make-up ilimbidi aanze kujifunza jinsi ya kutengeneza make-up hizo za kutisha kupitia mtandao wa YouTube kwani alikuwa hana pesa ya kujifunza sehemu nyingine ilikuwa ni gharama sana.

Nikataka kujua kama aliwahi kupita kwenye darasa lolote nchini Nigeria kuhusu aina hiyo ya make-up lakini mrembo wetu wa leo akasema hajawahi kwa sababu lengo lake ni kwenda kimataifa zaidi na hamini kama Nigeria angeweza kupata elimu hiyo ya kumfikisha kimataifa, lakini alijitahidia akapata somo la aina hiyo nchini Canada ambapo aliweza kupata uelewa mpana zaidi kuliko ambao angepata nchini Nigeria.

Lakini pia hakukaa kinyonge alikuwa anajitahidi sana kuwafatilia watu wanaofanya aina hiyo ya make-up ili aweze kuelewa wanafanya vipi hadi kuwatengeneza watu muonekano mwingine.

As you know me, huwa sichoki kuuliza kwa niaba yako, nikataka kujua mbinu na njia anazotumia katika kutengeneza watu akanitajia kifaa kimoja kinaitwa Silicone ya make-up, powder, huku akieleza kuwa vifaa vya kutengeneza make-up hizo vinauzwa kwa bei kubwa sana ndio maana yeye anawatoza wateja pesa ndefu pia huku akiwataka wateja wasilalamike wakitozwa pesa hizo kwani ni bei na ngumu kuvipata.

Upande wa make-up nyingine pia amekuwa akifanya kama vile editorial make-up , beauty make-up, lakini kwa sasa ameamua ku-concetrate na Arseface make-up ili akuwe zaidi katika eneo hilo.
Kila mtu huwa na changamoto zake kwenye kazi anazofanya , kwa upande wake anadai kuwa anakutana nazo kwa actors akiwa anawafanyia make-up muda mwingine wanakuwa wabishi kufanyiwa aina fulani ya make-up na kumpangia masharti.

Maongezi yalikuwa mengi sana , ikafika time nikamuuliza watu wanavyo mchukulia nchini Nigeria kwa kile anachofanya , akadai kuwa aina hiyo ya make-up Nigeria bado haijafahamika sana kwa hiyo watu wakiona wanashangaa sana, japo najua hata wewe unayesoma saa hii ukipata muda pitia kwa Instagram page yetu naajua utashangaa kwani vitu viko kama uhalisia.




Wale waoga wa movie za kutisha Abaeme anasema kuwa katika kazi zake zote anazipenda lakini ya kutengeneza mazombi huwa anaenda zaidi yaani kwa kifupi anadai anapenda sana kumtengeneza mtu aonekane anatisha.

Usipate shida ili uweze kuona zaidi kazi ambazo amewahi kufanya just go and watch movie alizofanya kazi kama vile “Far from home”, “Setup 2”, “Eagle Wings”, “Sugar” na nyingine nyingi.

Mwisho kabisa Abaeme anandoto ya kwenda mbali zaidi kikazi anatarajia kufika Hollywood.

So this weekend tunaimaliza na our beautifully Abaeme all the way from Nigeria… Tchaooo till next Friday.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags