Abadili mwili wake ili afanane na viumbe wa ajabu

Abadili mwili wake ili afanane na viumbe wa ajabu

Kama ilivyo kawaida kwa baadhi ya binadamu kuwa na tabia ya kujaribu kila jambo, hata yale ambayo wengine wanadhani ni magumu kufanyika, leo hii mfahamu raia wa Ufaransa aliyefanya upasuani mara nyingi zaidi kwenye mwili wake ili afanane na Black Alien.

Wafuatiliaji wa #movie jina la #Aliens litakuwa si geni kwenu, kuhusu viumbe hao watu wengi huamni na kuwaita viumbe wa ajabu kutoka sayari nyingine kutokana na muonekano wao, kama hukuwahi kuvutiwa na viumbe hao, fahamu kuwa wamemvutia sana Anthony hadi kufanya mabadiliko ya mwili wake.


Anthony Loffredo kutoka Ufaransa, ndiyo mwanaume ambaye amechora tattoo sehemu zote za mwili wake, amekata pua, masikio, baadhi ya vidole, ametenganisha kati ulimi wake na kukata mdomo wa juu ili kuwa kama Aliens.

Hajaishia hapo tu ukiangalia uso wake utaona vinundu ambavyo vimetokana na vipandikizi alivyoweka kwenye uso wake, upande wa paji la uso kukatika kwenye mfupa wa shavu ameweka mipasuko, macho nayo hajayaacha salama ameyabadili na kuwa na rangi ya muonekano tofauti kabisa na awali.

Hayo yote alianza kuyafanya kwanzia asilimia moja hadi sasa amefanikiwa kufikia asilimia 57 za mabadiliko yake, hivyo basi bado asilimia 43 ili awe na muonekano sawa kabisa na #Aliens


Anthony ambaye kwa sasa jina lake maarufu ni The Black ALIEN, alizaliwa mwaka 1988 kutokana na juhudi zake za kufanya mabadiliko ya mwili wake ameendelea kupata umaarufu hadi kufikisha followers 1.3M kwenye mtandao wa #Instagram, licha ya maneno mbalimbali ya watu Anthony anadai kuwa hayumbishwi na maneno hayo bali anafanya mabadiliko yake ili kukamilisha furaha yake






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags