Aamrishwa kumlipa mpenzi wake kwa kumuumiza moyo

Aamrishwa kumlipa mpenzi wake kwa kumuumiza moyo

Mwanamke mmoja nchini Uganda aliyefahamika kwa jina la Fortunate Kyarikunda ambaye aliuumiza moyo wa mchumba wake Richard Timwine ameamrishwa na mahakama kulipia hasara za kifedha kwa uchungu wa kisaikolojia.

Mahakama ya Kanungu ilisema kuwa Richard Tumwine alilipa shilingi milioni 9.4($2,550; £2,060) kwa ajili ya masomo ya sheria ya mwanadada Fortunate Kyarikunda, pesa ambazo sasa atatakiwa kuzilipa pamoja na gharama za kesi.

Kwa kusitisha uchumba wao baada ya miaka minne, Hakimu Asanasio Mukobi aliamua kuwa Fortunate alikiuka ahadi na kusababisha madhara kwa Tumwine.

Mahakama hiyo ilieleza kuwa "isiyo na maana, upotoshaji na ulaghai" kwa mshitakiwa kudai kuwa wazazi wake walimwambia asiolewe na mwanaume mzee sana, ikisema" alikuwa na wakati wote wa kukataa maombi ya mapenzi mapema na kuepuka kutumia pesa zake."

Haijulikani iwapo Bi Kyarikunda atakata rufaa dhidi ya hukumu.

Wakosoaji katika gazeti la Monitor wanaeleza kwamba hukumu ina kasoro kwasababu uchumba ni tofauti na ndoa ambayo inakubalika kisheria.

Aidha wakati huo huo Sheila Kawamara, kutoka kikundi cha utetezi wa wanawake ED EASSI, anaonya kuwa wakati mwingine huwa kuna hali za unyonyaji ambapo mwanaume humpatia pesa mwanamke kwa sharti kuwa atamuoa.

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags