Ofisi ya Umoja wa Mataifa (UN) inayosimamia Dawa za Kulevya na Uhalifu (UNODC) imesema kuna kasoro kadhaa katika kuripoti kuhusu biashara hiyo haramu na huenda idadi ya dawa hizo zisizofaa ikawa juu zaidi ya ilivyo kwenye takwimu zilizopo
UN imetoa angalizo hilo kupitia ripoti kuhusu biashara haramu ya bidhaa za matibabu
Kati ya Januari 2017 hadi Disemba 2021, takribani tani 605 za bidhaa za matibabu zilikamatwa Afrika Magharibi katika Operesheni za Kimataifa na ripoti ya hivi karibuni Shirika la Afya Duniani inaeleza kuwa kuna vifo 267,000 kila mwaka vinavyohusishwa na matumizi ya dawa za Malaria zisizokidhi vigezo.
Leave a Reply