50 Cent atia mguu ugomvi wa Chris Brown na Quavo

50 Cent atia mguu ugomvi wa Chris Brown na Quavo

Rapa kutoka nchini Marekani 50 Cent ameingilia bifu la msanii Chris Brown na Quavo kwa kusema bifu hilo linaingia katika hatua mbaya ambayo itaenda kuharibu biashara ya muziki.

Kufuatia bifu zito linaloendelea kati ya marapa hao 50 Cent, ameandika ujumbe huo katika mtandao wa X (zamani Twitter) “ugomvi huu sasa unaingia kwenye hatua ya tofauti” .

Wawili hao wamekuwa katika muendelezo wa bifu lao ambapo kila mmoja alikuwa akitoa wimbo kwa ajili ya kumchana mwenzake.

Ikumbukwe kuwa hivi karibuni Chris Brown amedaiwa kuwa alinunua tiketi za viti vyote vya mbele kwenye moja ya show ya hasimu wake Quavo ili msanii huyo aonekane hajajaza ukumbi.

Bifu la Quavo na Brown lilianza mwaka 2017 baada ya Quavo kudaiwa kutoka kimapenzi na aliyekuwa mpenzi wa zamani wa Brown aitwaye Karrueche Tan.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags