50 Cent Atema nyongo  siku ya Baba duniani

50 Cent Atema nyongo siku ya Baba duniani

YES!!! Moja kati ya suala ambalo limeibua mjadala huko mitandaoni ni hili hapa linalohusu maadhimisho ya siku ya baba duniani ambapo siku hiyo hutambuliwa kila ifikapo tarehe 19 mwezi juni ya kila mwaka.

Sasa bwana kutokana na siku hiyo Msanii kutoka nchini Marekani 50 Cent ameachia ujumbe mahususi kupitia mtandao wake wa kijamii kuhusiana na siku hiyo iliyoadhimishwa juzi.

 "Siku Ya Baba Sio Sikukuu Kabisa, Hata Ukiona Post za matangazo Huko Kwenye Mitandao Ya Kijamii Utaona Wameweka Screwdriver, Lakini Pia Michoro Inayoonesha Vifaa Vya Kazi Ikiwa Sehemu Tu Ya Kuwatakia Baba Wote Sikukuu Yao...Sisi Kinababa Hatupatiwi Vitu Vya Thamani Katika Siku Yetu Hii Lakini Kwenye Siku Ya Mama Duniani Utaona Sisi Wababa Tunawapatia Maua, Card Na Nk. ..lakini Sisi Wababa Tunapewa Kitu Gani Zaidi Tu Ya Kutumiwa Text Na Kutakiwa Sikukuu Hii, Meseji Inayokukumbusha Tu Majukumu Yako Yakuendelea Kutuma Hela " - 50 Cent

Ebwana eeeh!! Unayapa asilimia ngapi maneno ya 50Cent? Dondosha comment yako hapo chini.


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Saphinia Suleiman

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, career, skills development and technology.


Latest Post