50 Cent amwaga cheko baada ya kushinda kesi

50 Cent amwaga cheko baada ya kushinda kesi

‘Rapa’ kutoka Marekani 50 Cent amefurahia kushinda kesi iliyokuwa ikimtaka kulipa Sh 2.6 Trillioni hii ni baada ya kudaiwa kuiba stori ya muuza madawa ya kulevya aitwaye Holand na kuitumia katika filamu yake ya ‘Power’.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram wa 50 ame-share taarifa ya ushindi wa kesi hiyo aliyokuwa akikabiliana nayo kwa muda mrefu.

Utakumbukwa kuwa mwaka 2021 Holand alimshitaki 50 akidai kuwa ‘rapa’ huyo aliiba stori ya maisha yake na kutumia kwenye filamu yake ya ‘Power’ hivyo basi aliamua kupeleka shauli hilo mahakamani kwa lengo la kudai fidia.

Mbali na kudai fidia, pia mwaka 2023 alifungua kesi nyingine kwa 50 akidai kuwa msanii huyo alikodi wauaji kwa ajili ya kumuua kutokana na kushindwa kulisaficha jina lake katika kesi hiyo ya kuiba stori ya maisha yake.

Filamu ya ‘Power’ ni tamthilia ambayo ilikuwa ikielezea maisha wa wahalifu iliyotayarishwa na Courtney A. Kemp akishirikiana na Curtis '50 Cent' Jackson huku ikianza kuoneshwa kwa mara ya kwanza mwaka 2014.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags