30 wajeruhiwa baada ya treni ya abiria kuacha njia

30 wajeruhiwa baada ya treni ya abiria kuacha njia

Na Asha Charles

Takriban watu 30 wamejeruhiwa baada ya treni ya abiria kuacha njia magharibi mwa Uholanzi iliotokea siku ya jumanne.

Huduma za dharura zinasema ajali hiyo iliotokea usiku baada ya treni iliyokuwa ikisafirisha takriban watu 50 kugonga vifaa vya ujenzi  karibu na kijiji cha Voorschoten.

Waokoaji na madaktari sasa wanafanya kazi katika eneo la tukio, kusaidia majeruhi,  Katika taarifa yao ya hivi punde huduma za dharura zinasema waliojeruhiwa vibaya wamepelekwa katika hospitali, huku wengine wakipatiwa matibabi katika makazi yalio karibu.

Aidha gazeti la NRC limeripoti kuwa hakuna treni iliyokuwa ikisafiri kwa sasa kati ya The Hague na Leiden kwa sababu ya ajali hiyo kuziba njia.

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags