Zuwena wa Daimond si video vixer tu hadi kwenye kuimba yupo vizuri

Zuwena wa Daimond si video vixer tu hadi kwenye kuimba yupo vizuri

Bhana bhana!! Weekend nyegine ya kibabe tuna kutana tena na wanetu kubadilishana mawazo na kujuzana mambo kadha wa kadha mambo yanayoendelea katika burudani na michezo.

Hivi ulishawahi jiuliza au kuchunguza inakuaje mavideo vixer wengi wakishatoka basi wanakimbilia kuimba yawezekana video vixer ndio njia ya kutokea kimuziki wa kibongo.

Lakini Mungu si athumani bana wakishaingia huko upande wa pili wanapata umaarufu sana kuliko awali hapa, mfano mzuri wa video vixer ambao wameingia katika uimbaji na kuupiga mwingi katika muziki akiwemo Gigy money, Ammber Lulu na wengine wengi.

Kumekuwa na minong’ono mingi kupitia mitandao ya kijamii kuhusiana na suala la mavideo vixer wa kikimbilia katika uimbaji, leo tumekusogezea video vixer ambae ametrend miezi kadhaa ya nyuma na sasa ana tarajia kuachia ngoma yake ya kwanza.

Recho Elias wengi wenu wanamtambua kama Zuwena wa Daimond ambae aliupiga mwingi na kujulikana zaidi baada ya yakuwa video vixer, katika video ya msanii mkubwa anetingisha reality show ya ‘Young famous’ Daimond Platnamuz, katika nyimbo ya Zuwena.

Kupitia ukubwa wa video hiyo basi bhana  mwanadada huyu ndipo akapachikwa jina la Zuwena na kujizolea umaarufu mjini.

Team ya Mwananchi Scoop tuliweza kupiga stori na Zuwena kwa upande wake jambo la kuingia kwenye muziki wakati yeye ni video vixer kwa upande wake analichukuliaje amefunguka na kueleza kuwa

“kwasasa sina cha zaidi cha kuongea kuhusiana na mambo hayo, lakini mashabiki zangu watarajie ngoma mpya kutoka kwangu ambayo nisharecord na nimeshafanya video ila haikuwa rahisi mwanzoni kuingia studio na kurecord nyimbo kwahiyo nawaomba tena Watanzania wanishike mkono na wanipokee mimi kama Zuwena ”alisema Recho

Wengi wenu mlikuwa mlimtambua mwanadada huyo kupitia wimbo wa Zuwena, lakini struggule zake za kujitafuta zilianza miaka 10 iliopita na alishawahi kufanya kazi na wasanii mbalimbali lakini hakuweza kutoka.

Kama tunavyojua katika kila harakati za mafanikio lazima kuwe na changamoto mwanadada huyo alifunguka kupitia Mwananchi Scoop na kueleza kuwa

“Changamoto zipo nimepitia changamoto mbalimbali ikiwemo kuto kukubalika kwa haraka  katika kazi zangu na watu wanao nizunguka”alisema zuwena

Kama kawaida yetu huwa hatunaga mba mba mba tukaona isiwe tabu wacha tupige nae stori mbili tatu kuhusiana na maisha yake.

Sambamba na hayo anaifurahia kazi yake na anafuraishwa na vitu mbalimbali kwa mfano kufika sehemu ambazo hapo awali ilikuwa sio rahisi kwa mtu kama yeye kuweza kufika.

 

Kama tunayojua bwana kila mtu anatamani apate mtu ambae atamsaidia ili kutimiza ndoto zake kwa upane wake amesema kama kuna mtu anataka kumsaport katika sanaa yake basi katika swala la kuimba atafurahia sana anasema

 “Ikitokea nimepata meneger ambae atanisimamia kwaajili ya kufanya muziki ntafurahi sana, yaani natamani mno mtu anisaport katika hilo”alisema Zuwena.

Ndoto kubwa ya Video vixer huyo ni kufika mbali kimuziki ili na yeye aje kuwasaidia wengine ambao watatamani kuwa kama yeye katika Sanaa, anatamani kufanya kama alichofanyiwa yeye na Diamond.

Licha ya kuwa video vixer na muimbaji mwanadada huyo ni mama wa mtoto mmoja na ni muumini wa kikrisho anaipenda dini yake na kuiyamini pamoja na kufanya mambo mengine ya kidunia lakini Imani yake kwa Mungu ni kubwa.

Ebana! kwaleo niishie kusema kwamba safari moja huanzisha safari nyengine katika utafutaji hayo yote ni moja ya kutafuta maokoto, so tupambane haijalishi watu watakuchukulia vipi.

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags