Zuchu: Msizichukulie poa team za soccer

Zuchu: Msizichukulie poa team za soccer

Mwanamuziki #zuchu ametaoa angalizo kwa wasanii wanaopata nafasi ya kutumbuiza kwenye matamasha ya 'timu' za mpira wa miguu Tanzania kutochukulia poa nafasi hizo na kufanya kweli.

Zuchu ameyasema hayo leo kupitia ukurasa wake wa Instagram ikiwa ni dakika chache tu baada ya msanii wa muziki wa Bongo Fleva Alikiba kumaliza kutumbuiza kwenye tamasha la Simba Day.

Vilevile msanii huyu wakike anayesumbua kwa sasa nchini alisema wasanii waige kwenye kile alichokifanya yeye kwenye tamasha la Simba Day mwaka jana ambapo anadai lilikuwa moja ya tamasha bora la timu  kuandiliwa na mwanamke kuwahi kutokea nchini.

“Angalizo kwa wasanii, hizi ndio SUPER BOWL zetu tusizichukulie poa..Maana Team za Soccer zimetuheshimisha hivyo nasi ni vyema Tuziheshimishe…Ikumbukwe kuwa Hii ni moja kati Ya SIMBA DAY KUBWA kutokea Kwenye historia ,Upangiliaji wa show, mavazi Na Kila kitu .Na ilifanywa Na Mwanamke Na mwanamke mwenyewe ni Mimi”






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags