Zoleka aliandika orodha ya watu asiotaka wafike kwenye msiba wake, Ex wake yumo

Zoleka aliandika orodha ya watu asiotaka wafike kwenye msiba wake, Ex wake yumo

Inadaiwa kuwa mjukuu wa Nelson Mandela, Zoleka aliyefariki wiki iliyopita kwa ugonjwa wa ‘kansa’  aliacha wosia ambao ametaja baadhi ya watu ambao hakutaka wafike kwenye mazishi yake huku akieleza sababu kubwa ni kumnyanyasa kijinsia.

Kupitia oradha hiyo baadhi ya watu walishangazwa na kuwepo kwa jina la mumewe wa zamani anayejulikana kwa jina la Thierry Bashala ambaye alizaa nae watoto wawili.

Licha ya Bashala kuwa katika orodha hiyo alitumia wasaa wa kuomboleza Instagram kifo cha mama watoto wake huyo.

Aidha Zoleka aliwataja pia baadhi ya ndugu ambao waliwahi kumnyanyasa kijinsia na hakutaka wasogelee mazishi yake. Katika orodha aliyoiandika Zoleka majina ya aliyowekea alama ya nukta au ‘doti’ ndio waliowahi kumnyanyasa kijinsia.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags