Zingatia haya wakati wa kubandika kucha bandia

Zingatia haya wakati wa kubandika kucha bandia

Ni siku nyingine tena tunakutaka kupitia dondoo hii ya fashion ili kuweza kujuzana mambo mbalimbali kuhusiana na masuala mitindo, urembo na mavazi ambayo najua uwenda unayajua ila mimi nakujua zaidi.

Msomji wangu mpendwa leo tutaangalia mambo ya kuzingatia wakati wa ubandikaji kucha, ambao umekuwa ukishamiri kila kukicha hasa kwa upande wa wanawake.

Tunona kila siku ubunifu katika suala la urembo linazidi kukua, hasa urembo wa kucha wabunifu wamekuwa wakitafuta mbadala wa watu wasioweza kufuga kucha na kupendeza waweze kufurahi kucha zao na ndipo kubuni kucha hizi za kubandika.

Ubandikanji kucha umekuwa ukifanyika kwa aina tofauti tofauti, ila cha muhimu unachopaswa kuzingatia ni kwamba unapenda kucha zako ziwe katika muonekano gani, pia unapaswa kutambua rangi itakayoweza kuendana na ngozi yako ya kucha ili uvutie zaidi.

Unashauriwa kajua ni aina gani ya gundi itakayotumika kuwekwa katika kucha ili usipate madhara, pia wakati wakutoa hakikisha unaweka mikono yako yenye kucha hizo bandia katika maji ya uvuguvugu na kubandua taratibu ili usipate madhara.

Aidha inaelezwa kuwa zipo dawa ambayo utumika kubandua kucha iliyobandikwa pimdi utakapokwenda kwa mbandikaji lazima atakuwa nayo.

Basi hayo ni kwa uchache tu endelea kutufatilia ili kuweza kujifunza mambo mengi zaidi.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm


Latest Post

Latest Tags