Zimbabwe Surua bado ni kichomi yaua watoto 80

Zimbabwe Surua bado ni kichomi yaua watoto 80

Mlipuko wa ugonjwa wa Surua nchini Zimbabwe umesababisha vifo vya watoto 80 tangu mwezi Aprili na mamlaka za nchi hiyo zimesema maradhi hayo yamesambaa kote nchini humo.

Taarifa iliyotolewa na waziri wa afya wa Zimbabwe Jasper Chimedza imesema hadi kufikia Alhamisi iliyopita visa 125 vya Surua vimethibitishwa huku visa vingine 1,036 vinavyodhaniwa kuwa Surua vimeripotiwa.

Serikali ya Zimbabwe inasema mkusanyiko wa waumini wa kanisa moja nchini humo ndiyo chanzo cha kusambaa kwa maradhi hayo yaliyoripotiwa kwa mara ya kwanza mnamo Aprili 10.

 Waziri Chimedza amesema visa vingi vimeripotiwa katika jimbo la mashariki la Manicaland na wengi ya walioathirika ni watoto wenye umri wa kati ya miezi 6 hadi 15 kutoka jamii ya waumini wa kanisa hilo ambao hawakupatiwa chanjo kutokana na imani za kidini.

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags