Zijue mbinu na namna za kuzingatia katika uvaaji wa pete

Zijue mbinu na namna za kuzingatia katika uvaaji wa pete

Niajeeeh!!! Another weekend vipenzi vyangu na watu wangu wa nguvu kama ilivyo kawaida yetu ni muhimu kwetu kupitia dondoo za fashion kila wiki kwasababu tunajua mitindo ni maisha ya kila siku tangu zama za kale.

Leo katika uwanja wa fashion tunakusogezea namna ya kuzingatia uvaaji wa pete kwaajili ya urembo.

Kwanza kabisa Pete ni pambo maalum ambalo linaweza kuongeza uzuri wa mtu kwa urahisi kwa kuzingatia sehemu za mwili wetu tunazotumia zaidi kama mikono.

Hata hivyo, kuna aina nyingi tofauti za pete na mitindo ambayo kuchagua moja kamili inaweza kuonekana kama kazi kubwa.

Lakini pete ni uamuzi wa mtu binafsi, hivyo mwisho wa siku, ni juu yako jinsi unavyochagua kuivaa tunajua watu wengine hawapendi kuvaa pete mh! ila kwa dunia ya leo watu wamechangamka na fashion yaani kumi kwa moja asie penda kuvaa pete.

Ukiwa unatafuta msukumo wa ziada wa kufuata miongozo ya mitindo, unapaswa kuzingatia kuwa itakuwa bora kwa pete zako kulingana na mavazi yako mengine, inatokea mtu anavaa pete bila ya mapangilio au eneo husika analokwenda.

Kama ukiwa unaenda ofisini huwezi ukavaa pete nyingi mkononi utaonekana tofauti kidogo hivyo inakubidi utafute pete yako simple tu kama ni moja au mbili.

Ili kuhakikisha kuwa pete zako hazielemei mwonekano wako wa jumla, ni muhimu vile vile zilingane na vito vyako vingine, haswa saa, kwani ziko karibu nazo.

Pete iboreshe mwonekano wake, sio kuifanya kama uonekane wa ajabu.

Ni kwa upande wa mkono gani wa kuvaa pete yako hiyo ni juu yako bila kuhusishwa hiyo haitumiki kwa pete za ushiriki na pete za harusi, ambazo zinapaswa kuvikwa kwa mkono wa kushoto la hasha kwa zile za urembo.

Lakini pete yako inatakiwa kuwa na muonekano mzuri uvaapo kidoleni nakuwa na mpangilio kutokana na umbo au saizi ya kidole chako, kuna mambo ya kuzingatia ilipete ikikae vizuri katika kidole chako.

TAMBUA MABADILIKO YA SIZE YA VIDOLE VYAKO

Hapa mpendwa wangu unatakiwa usikalili saizi unayo vaa pete kila siku kwa sababu vidole vyetu hubadilika saizi kulingana na hali ya hewa kuna kipindi unaweza kunenepa au ukapungua hali hizi zinatokea kama kwa kile tunachokula, au kutokana na kufanya kazi kwa mikono yetu sana.

Lazima ujue mwili unapoongezeka au unapo pungua na vidole navyo vinakuwa au vinapua kutokana na mabadiliko ya mwili wako hivyo itakulazimu kubadilisha pete.

UKUBWA WA PETE

Unapaswa kufanya kazi na sonara mwenye uzoefu ili kupata ukubwa wa kidole chako kitaaluma na sizungumzii kwenda kwenye duka la vito ambayo yana saizi ya plastiki na mshirika wa mauzo asiye na uzoefu.

Wakati utakuwa umevaa kitu cha maana na cha gharama kubwa kama bendi ya harusi, unataka kuhakikisha kuwa unafanya vizuri lakini ikiwa pete yako haina gharama ina kupasa ujue saizi yako.

Usichopaswa kufanya ni kutafuta tu mbinu za kupima pete mtandaoni kisha ujifanyie mwenyewe bila kwenda watu wenye utaalamu itakugharimu.

UMBO LA KIDOLE

Ikiwa una vifundo vidogo, au vidole vya tipi pete yako itabidi iwe laini zaidi na ikiwa una vifundo vikubwa zaidi, utakutana na tatizo la pete yako kuwa imelegea sana chini ya kidole chako.

Pia ikiwa imefungwa sana, itakuwa ina maumivu wakati wa kuvaa zaidi na mikono yako itavimba kutokana na unyevu au kitu kingine.

PETE ISILEGE SANA KIDOLENI

Bila shaka, wewe pia hutaki pete ambayo hutokaa kwa urahisi sana  jambo ambalo mtu yeyote halitamvutia hasa akiwa mbele za alaiki ya watu na itakunyima confidance hivyo ni vizuri pete ikakufiti ili ikupe muonekano mzuri katika mitindo yako ya kuvaa mwanetu.

Basi tu nikwambie weekend yetu katika fashion inaisha hivyo tutakutana next week kujuza mengine ila nikukumbushe tu mitindo (fashion) ni sehemu ya maisha ya kila siku usikubali kupitwa wewe.

 

 

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags