Nafahamu kuwa mwanafunzi wengi hasa wa vyuo wana vitu vingi vya kufanya ikiwemo masomo, mitihani hata kufurahi pamoja na wenzako.
Hata hivyo ni wazi kuwa ni ngumu mwanafunzi kuanza biashara ukiwa chuoni ila tambua kuwa ukifanya biashara inaweza kukusaidia kuweka msingi kama unataka kuwa mfanyabishara mkubwa mbeleni.
Jackline Rutta ni mwanafunzi wa Chuo cha Uhasibu (TIA) kilichopo jijini Dar es Salaam ameamua kupiga story na mimi na ametueleza biashara ambazo mwanachuo anaweza kuzifanya akiwa bado yupo chuoni.
Rutta ambaye anachukua masomo ya Human Resource Management katika chuo hicho anasema kupitia MwananchiScoop ataeleza aina mbalimbali za biashara ambazo Mwanafunzi anaweza kuzifanya na akajiingizia kipato.
Anasema kabla ya kuanza kufikiria baishara mtu anapaswa kutengeneza mtandao wa watu ambao atawatumia baadaye katika biashara zake.
Rutta anasema biashara ambazo mwanachuo anaweza kuzifanya ni hizo zifuatazo chini:
Kuuza Airtime
Anasema mwanafunzi anaweza kufanya biashara ya miamala ya kifedha kama M-pesa, Tigo pesa, Airtel Money, TTCL na Eazy.
“Wote tunafahamu kuwa wanafunzi wa chuo wanamatumizi sana ya simu hivyo ukiamua kufanya baishara hiyo ya kuuza airtime lazima utapata tu fedha, ila unaweza kujiongeza ukauza na vifaa vingine kama flash zenye ubora wa hali ya juu hata kujafanya usajili wa laini za simu mitandao mbalimbali,” anasema
Anasisitiza kuwa biashara ya uuzaji wa airtime ni nyepesi kwa kuwa wateja ni wale wanafunzi wanaokuzunguka darasani, lecture room, kwenye discussion hata disco.
Kufanya Printing
Rutta ambaye kwa sasa anafanya baishara ya kuuza nguo anasema biashara ya printing inafaida kubwa sana kama mwanafunzi atahamua kuifanya.
“Unachotakiwa kama unayo laptop, jinunulie kaprinta kako hata ka Sh. 100,000 kaweke bwenini na uwatangazie wenzako kwamba unaprint kwa bei poa kuliko steshenari za jirani, mwanangu lazima tu watu watakuja kwako,” anasema
Kuuza nguo mitandaoni
Anasema yeye biashara ya kuuza nguo mitandaoni ndiyo anayoifanya na imekuwa ikimletea faida na kuwapunguzia wazazi wake majukumu ya kumuhudumia fedha za chuo.
Rutta anasema mwanafunzi yeyote anaweza kutumia simu janja yake kuanzisha biashara yoyote ile mitandaoni ikiwemo ya uuzaji wa nguo.
“Kule kwenye simu zetu tunapoweka status tunaweza sasa kutumia kwa kuposti nguo tunazouza au hata simu pia unaweza kuuza, mwanangu ukifanya hivyo utakuja kuniambia wateja utakaopata, cha msingi ni kutambua wateja wako wanapenda nguo za aina gani,” anasema
Uandishi wa Vitabu
“Hapa napo kuna faida ukizingatia kwa wale mnaopenda simulizi za mahusiano, umbea, udaku, au hata visa na mikasa mbalimbali ya kimaisha anza kuandika hizo mambo kisha hifadhi kwenye laptop yako au flash disk anza kuuza kwa wachapishaji.
“Inaweza kuwa short story au series ili mradi iwe ya kuvutia tu Mwanangu mwenyewe nakwambia lazima utapata fedha tu,” anasema.
Mambo ya kuzingatia
Rutta anasema kabla mwanafunzi hajaanzisha biashara chuoni, anapaswa kuzingatia mambo muhimu yafuatayo
Anasema kwanza anapaswa kutambua kuwa hawezi kufanya kila kitu peke yake, anahitaji msaada kutoka kwa watu, iwe roommate au mtu utakayemuajiri.
“Zingatia sababu ya kuanzisha biashara na malengo uliyonayo kuhusu hiyo biashara, je unataka tu hela ya kula au unataka hiyo biashara iwe kitu cha muda mrefu hata ukimaliza chuo ikuendeleze mtaani? Na kama ni hivyo una malengo gani ya kuikuza?,” anasema
Pia anafafanua kuwa kabla ya kuanzisha biashara mwanachuo anapaswa kujua jinsi ya kubalance muda vizuri kati ya masomo yake, biashara na maisha yake ya kijamii.
“Tambua tu kufeli ni sehemu ya kujifunza, biashara inakufanikiwa na kujifunza. Usijisikie vibaya au aibu kufeli, usiogope kufeli, unajifunza vitu vya muhimu ambavyo usingeweza kujifunza kama unsingejaribu.
“Zingatia kilichokupeleka chuo kama namba moja kwako, na hicho ni kusoma. Wewe ni mwanachuo mwenye biashara sio mfanyabiashara anayesoma chuo,” anasema
Hata hivyo Rutta anasisitiza kuwa sio mara zote biashara zinafanikiwa, ila mtu anapoanza mapema na huku anaendelea na masomo madhara yake sio makubwa kuliko ukiwa nyumbani unafanya biashara hiyo hiyo halafu ikakushinda.
“Unapoendelea kujifunza unatengeneza taaluma yako ya baadaye kibiashara. Watu wengi watategemea ushindwe, ila kushindwa huko kunakuongezea uzoefu wa kufanya na kuepuka makosa baadaye. Unahitaji ubunifu na kutokukata tamaa pale mambo yanapokuwa hayaendi vizuri,” anasema.
Aidha anasema licha ya kufanya baishara ni vizuri hapo baadae mtu akmaliza chuo akajiendeleza kielimu kuhusiana na masuala ya biashara ili asijekupoteza fedha na muda.
Hivyo Rutta amesema mwanafunzi anapokuwa chuoni ajifunze kupitia mafunzo madogo madogo yanayohusu biashara na afanyie utafiki na mazoezi namna ya kufanya hizo biashara.
“Ili utakapotoka chuoni ujue ni jambo gani hasa unataka kuliendeleza kibiashra baada ya kujifunza na kujaribu aina mbalimbali za biashara ukiwa chuoni. Utajikuta unatengeneza taaluma ambayo ndio yatakuwa maisha yako hapo mbeleni,” anasema
Kupitia Makala hii kijana wenzangu wala hata usiogope kuanzisha biashara chuoni, usiogope hasara, unajifunza mengi kwa kufanya kuliko kuwaza tu au kuona wengine wakifanya.
Ila zingatia tu kuwa ni muhimu pia kufocus kwenye masomo pia hata kama hela inaingia vizuri kwenye biashara.
Leave a Reply