Zifahamu faida za kula mboga za majani

Zifahamu faida za kula mboga za majani

Hivi sasa kumekuwa na fikra potofu katika jamii za kiafrika kuwa mboga za majini ni kwa ajili ya maskini tu.

Watu wengi hasa huko mitaani ili waonekana wanafedha za kutosha basi upendelea kula mboga kama kuku kwa wingi, nyama, maini, soseji na uonekana kuwa wana fedha nyingi ndio maana wanamudu kula vyakula hivyo.

Hata hivyo wanasahau kuwa ulaji wa mboga za majani una faida nyingi za kiafya kama anavyotueleza mtaalamu wa msuala ya Lishe kutoka Haliamshauri ya Temeke Dk, Charles Malale.

Alisema mboga za majani zina faida nyingi za kiafya hii ni kutokana na asili yake ya kuwa na vitamin wa wingi, madini kwa wingi na zinasaidia kukinga mwili kwa magonjwa mbalimbali.

“Mboga za majani pia zinasaidia sana kupunuza uzito wa mwili kwa mtu mwenye uzito uliopitiliza kwani zinamafuta kidogo sana. Mafuta yake yanayenyushwa vizuri na joto la mwili kuliko mafuta yatokanayo na mboga za vitoweo vya nyama,” alisema Dk. Malale

Alisema mboga za majani zina nguvu ukaa kidogo sana kulinganisha na mboga zingine kama nyama na kuongeza kuwa nguvu ukaa inapokuwa nyingi mwilini kutokana na chakula zinakuwa mafuta mwilini ambayo mtu unenepa sana na uzito kuongezeka.

Dk. Malale alisema mboga za majani zinaongeza  maji kidogo kidogo mwilini kwa sababu zina madini ya sodium kwa wingi.

 

Pia alisema mboga hizo zinashibisha haraka na kujaza tumbo mapema kwa sababu ya umbirorojo au cellulose na zinaongeza  uhai au “vitality” kwa sababu zina virutubisho vingi muhimu kwa mwili.

“Embu fikiria siku 20 za kula mboga mboga tu na protein kiasi bila wanga au wanga kidogo sana, kumbuka mboga hizi zinaliwa zikiwa zimepikwa kidogo au zimetengenezwa kama kimiminika, fanya haya utakuja kuniambia matokeo yake,” alisema na kuongeza

“Kwa hiyo mboga za majani zina sifa zote za kukufanya upunguze uzito kwani zina vitamini nyingi sana na madini ambayo ni muhimu katika kuufanya mwili wako uwe na afya njema muda wote,” alisema

Anasisitiza kuwa mboga za majani zina kemikali rafiki kwa mwili kwa kuponyesha magonjwa na kuufanya uwe na kinga nzuri sdhidi ya magonjwa mengi.

“Mboga hizi pia hunyonya mafuta toka utumbo mwembamba kwa sababu ya nyunyuzi au umbijani rojorojo au cellulose ambayo zina nyunyuzi kwa wingi. Pia mboga hizi zina mafuta kidogo sana ambayo joto la mwili nyuzi 36.7 centigrade linayeyusha mafuta hiyo kwa urahisi sana,” alisema.

Hata hivyo alisema mboga za majani zina tu nguvu ukaa kidogo sana ukilinganisha na vyakula vingine. “Mafuta yatokanayo na mboga huwa hayagandi katika damu ndani ya mishipa ya damu tofauti na mafuta yatokanayo na mboga za nyama ambayo huganda na kuzuia damu ndani ya mishipa yetu ambayo husababisha vifo vya kushtukiza,” alisema na kuongeza.

 

“Mafuta ya mboga yanayeyushwa na kuuguzwa kwa hiyo hayakai mwilini katika mfumo wa mafuta “fat”. Mwili unakuwa si wa kunenepa bali unakuwa na afya nzuri yaani mwembamba na mrembo zaidi,” alisema.

Alisisitiza kuwa mboga za majani zina madini muhimu ya sodium ambayo upunguza maji mwilini.

“Mwili ukiwa na maji mengi unakuwa mnene na mzito kuliko kawaida yake. Kwa hiyo mboga mboga za majani ni muhimu kwa kupunguza maji mwilini na kupunguza uzito,” alisema.

Alimalizia kwa kusema mboga hizo zinazuia kuvimbiwa kuliko vyakula vingine na zinaongeza uhai kwa sababu ya sifa zake. Watu wanaoishi muda mrefu ni wenye kula mboga mboga kwa wingi.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm


Latest Post