Zari na shakibi wamaliza tofauti zao

Zari na shakibi wamaliza tofauti zao

Baada ya kuzuka sintofahamu kwa wanandoa Zari pamoja na mumewe Shakibi kuwa wameachana, wawili hao wamethibitisha kuwa wapo pamoja baada ya kuonekana Saudi Arabia.

Kupitia ukurasa wa Snapchart wa Zari ame-share video na picha mbalimbali akiwa na mumewe huyo, ambapo wapo Saudia kwa ajiri ya ibada ya Umrah.

Ikumbukwe kuwa wiki iliyoisha wawili hao walikuwa katika ugomvi na kupelekea kila mmoja kumu-unfollw mwenzake kupitia kurasa zao za Instagram, ambapo kufuatiwa na jambo hilo Shakibi Lutaaya alidaiwa kufungasha virago na kurudi nchini Uganda.

Licha ya kuzuka stori mbalimbali kwenye mitandao ya kijamii lakini hakuna yoyote kati yao ambaye amethibitisha kuachana kwao. Wawili hao walifunga ndoa Oktoba 3, mwaka jana nchini South Africa.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags