Zari na Shakib wadaiwa kuachana, Diamond atajwa

Zari na Shakib wadaiwa kuachana, Diamond atajwa

Mfanyabiashara Zari na mumewe Shakib wameripotiwa kugombana tena, hii ni baada ya mwanamuziki Diamond kutua Afrika Kusini kwa ajili ya kusheherekea siku ya kuzaliwa ya mtoto wake wa kwanza Tiffah.

Kufuatia na video zinazoendelea kusambaa mitandaoni Zari ameonekana kumlalamikia mumewe kwa kutomuamini licha ya kumchagua Shakib dhidi ya watu wengine wanaotamani kuwa naye kwenye mahusiano huku akifunguka kuwa mumewe huyo amekuwa akifikiria kuwa Zari bado anahisia za kimapenzi na Diamond.

Utakumbuka kuwa mkali wa ‘Komasava’ Diamond alikwenda Afrika Kusini Agosti 6, 2024 kwa ajili ya kusheherekea siku ya kuzaliwa ya binti yake Tiffa ambaye ametimiza miaka 9.

Hii sio mara ya kwanza kwa wawili hao kutengana mwanzoni mwa mwaka 2024 wanandoa hao waliripotiwa kutengana huku kila mmoja akimu-unfollw mwenzake kupitia kurasa zao za Instagram na Shakib kurudi kwao Uganda, lakini wiki chache baadae walirudiana tena.

Zari na Shakib walifunga ndoa Oktoba 3, mwaka jana nchini South Africa.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags