Zaidi ya waumini 20 wafariki njaa ili waende mbinguni

Zaidi ya waumini 20 wafariki njaa ili waende mbinguni

Polisi kutoka nchini Kenya wamepata miili 21 ya waumini wa kanisa la Good News International Church linaloongozwa na mchungaji Paul Mackenzie, ambaye anashikiliwa na polisi kwa madai ya kuwataka waumini wake kufa njaa ili kufika mbinguni kwa haraka, miili hiyo imegundulika eneo la Kilifi.

Polisi imesema miongoni mwa waliofariki na miili yao kupatikana ni watoto na huenda miili zaidi ikapatikana katika utafutaji wa miili unaoendelea kwa siku ya nne sasa.

Miili hiyo imepatikana baada ya maafisa wa ofisi ya DCI kuchimba makaburi mafupi yaliyokuwa kwenye ardhi ya Kijiji cha Shakahola Kaunti ya Kilifi.

Kiongozi wa kanisa la Good News International Church, Paul Mackenzie anadaiwa kuwalazimisha waumini wake kuanzia watoto wadogo hadi watu wazima kufunga kula chakula hadi kufa kama njia ya moja kwa moja ya kufika kwa muumba wao.

Aidha Mackenzie, ambaye kwa sasa yuko mahabusu huku uchunguzi dhidi yake ukiendelea, anadaiwa kuwa amefanya mgomo wa kula chakula akiwa mahabusu.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags