Zaidi ya watu 70 wafariki katika mkanyagano wa kupokea misaada ya ramadhani

Zaidi ya watu 70 wafariki katika mkanyagano wa kupokea misaada ya ramadhani

Takriban watu 78 wameuawa katika mkanyagano katika shule moja ilioko mji mkuu wa Yemen, wakati wa ugawaji wa misaada kwa ajili ya Ramadhani.

Shirika la habari la Reuters linaripoti kuwa mamia ya watu walimiminika katika shule hiyo kupokea michango ambayo ilikuwa takriban $9 (£7) kwa kila mtu.

Huku zaidi ya watu 300 wamejeruhiwa na 13 wakiwa katika hali mbaya, afisa wa afya mjini Sanaa alisema

Shirika la habari la Associated Press linawanukuu watu wawili walioshuhudia ambao walisema wapiganaji wa Houthi walifyatua risasi hewani katika kujaribu kudhibiti umati wa watu, wakionekana kugonga waya wa umeme ambao ulisababisha mlipuko. Hii ilisababisha hofu kwa watu mpaka kukanyagana.

Tukio hilo lilitokea wakati wa siku za mwisho za mwezi mtukufu wa waislamu wa Ramadhani, ambao huadhimishwa na kipindi cha kila mfungo.

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post