Zaidi ya watu 1000 wakusanyika kusheherekea uhalalishwaji wa bangi

Zaidi ya watu 1000 wakusanyika kusheherekea uhalalishwaji wa bangi

Zaidi ya watu 1000 nchini Ujerumani siku ya Jana wamekusanyika katika maeneo mbalimbali kusherehekea kuhalalishwa kwa matumizi ya bangi nchini humo.

Licha ya ruhusa hiyo watumiaji wameonywa kuvuta bangi karibu na maeneo ya michezo pamoja na shule huku wakiruhusiwa kubeba gramu 25 za bangi na kulima miche mitatu tu.

Ikumbukwe kuwa Februari 23 mwaka huu Bunge nchini humo liliidhinisha sheria hiyo ambayo imewaruhusu kutumia bangi watu waliotimiza miaka 18.

Hii inakuwa nchi ya tisa kuhalalisha bangi, ikifungua fursa mpya za biashara kwa makampuni ya bangi ya #Canada na #Marekani, ambayo bado yanasubiri kuhalalisha bangi.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags