Yusuph Mlela azindua duka la Ice Cream, afagilia tuzo za filamu

Yusuph Mlela azindua duka la Ice Cream, afagilia tuzo za filamu

Msanii wa filamu nchini, Yusuph Mlela ‘Mlelando’ amezindua duka la IceCream na kufagilia tuzo za filamu nchini kwa kusema uwepo wake utasaidia kurudisha hali na morali kwa wasanii kutengeneza kazi bora na zenye viwango.

Mlela ameyasema hayo hivi karibuni jijini Dar es Salaam wakati akizindua duka hilo lenye Ice Cream za radha tofauti tofauti maarufu kwa jina la Dr. Sweet.

Alisema tuzo hizo za filamu ambazo zimeandaliwa na Serikali ni kubwa na zinafanyika kwa mara ya kwanza hivyo anaimani kuwa zitarudisha hali na morali mpya ya utengenezaji wa filamu nzuri na bora hapa nchini.

“Kwa muda mrefu tasnia ilikuwa haina tuzo, ila sasa zimekuja  na kwa kuwa zimeandaliwa na Serikali watazisimamia vizuri, mimi binafsi nimeamasika kushiriki ndio maana nimepeleka filamu yangu, kwa hiyo tunasubilia siku mbili hizi kutangazwa majina ya watu walioteuliwa kuwania.

“Naamini kwa filamu niliyoipeleka na mimi nitakuwa mteule wa kuwania tuzo hizo. Ujue unapofanya vitu alafu hakuna tuzo ushindani unapotea hivyo tunaimani kupitia tuzo hizi watu watafanya kazi kwa bidii,” alisema Mlela

Hata hivyo alisema amehamasika kuzindua duka hilo, kwa kuwa yeye ni mpenzi wa Ice Cream hivyo watu wajitokeze kwa wingi katika duka hilo ili kupata radha tofauti tofauti.

"Mimi nimpenzi wa ice cream na nimeshakula sehemu nyingi lakini Dr Sweet ni sehemu ya tofauti na tunatoa huduma za kitofauti tofauti zaidi tofauti na sehemu zingine." alisema Mlela

Naye Meneja wa Dr. Sweet, Ayub Mohamed alisema katika duka hilo wametoa ajira kwa vijana zaidi ya 15 lakini nia yao ni kuhakikisha wanasambaa zaidi mkoani Dar es Salaam na kutoa ajira kwa vijana.

“Tumemchagua Mlela kuja hapa kwa sababu anapendwa na watu hasa vijana na amekuwa mtu mwenye ushawishi mkubwa kwa jamii,” alisema

 

 

 

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm


Latest Post

Latest Tags