Yusuph Mlela atoa siri kilichofanya achague sehemu ya kizikwa

Yusuph Mlela atoa siri kilichofanya achague sehemu ya kizikwa

Licha ya kuwa katika jamii inaonekana kama jambo la kutisha, kushangaza na kuogopesha akisikika mtu akizungumzia mazingira ya kuhifadhiwa kwake baada ya kufariki lakini kwa mwigizaji Yufuph Mlela mapema ametoa maagizo ya kuzikwa makaburi ya Kinondoni na siyo mwili wake kusafirishwa.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram aliandika, "Ikitokea nimefariki(nimekufa) mwili wangu utazikwa makaburi ya Kinondoni Ufipa(home) sisafirishwi popote,"

Mbali na kuandika ujumbe huo Mlela ameiambia Mwananchi Scoop kuwa sababu kubwa ya kuandika ujumbe huo ni kutotaka maiti yake igombaniwe.

"Hisia zimenituma nitoe ujumbe huo na ninamaanisha kweli, huwezi kujua siku nitayofariki duniani nimeandika ili hata siku nimefariki ndugu zangu wakataka kugombania sehemu ya kuzikwa nakuwa nimeamua wapi nizikwa ili nitoe utata.Maiti inatakiwa kuzikwa na siyo kusumbuliwa nataka kuzikwa sehemu ambayo nimezaliwa, nimekua na maisha yangu ninapoyaendesha,"amesema

Licha ya kuzungumza hayo amesema yeye ni mzima wa afya. 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Christina Lucas


Latest Post

Latest Tags