Young Killer: Mama yangu ndiyo mtayarishaji wa ngoma zangu

Young Killer: Mama yangu ndiyo mtayarishaji wa ngoma zangu

Msanii kutoka nchini Young Killer amewashangaza mashabiki wengi baada ya kuweka wazi kuwa mama yake mzazi ndiyo mtayarishaji wa nyimbo zake.

Young Killer kupitia ukurasa wake wa Instagram ameweka wazi swala hilo baada ya ku-share video akiwa na mama yake studio ambapo kulikuwa na kionjo cha wimbo huo uliotengenezwa na mama yake huku akieleza kuwa siku za hivi karibuni ataanza kuziachia kazi hizo.

Mwimbaji huyo wa hip-hop katika ‘posti’ zake za hivi karibuni amekuwa aki-share ‘picha’ akiwa na mama yake, na katika ngoma yake ya mwisho mtayarishaji wake alikuwa ni Wizzo808 wa ‘Stress free’ uliotoka mwezi mmoja uliopita.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags