Rapa Young Boy kutokea nchini Marekani amepangiwa kuachiwa huru Julai 27, 2025 baada ya kutumikia kifungo cha miezi 23 gerazani kwa kesi ya kumiliki silaha kinyume na sheria.
Rapa huyo ambaye jina lake halisi ni Kentrell D. Gaulden, alihukumiwa kifungo hicho kwa tuhuma za kumiliki bunduki ambazo zilihusika kwenye tukio la kushambulia mjini Louisiana Marekani.
YoungBoy amekuwa akiishi mji wa Utah tangu 2021 Alitumia zaidi ya miaka miwili chini ya kifungo cha nyumbani lakini alihamishiwa jela mwezi Mei 2024 baada ya maafisa wa polisi kuvamia nyumba yake na kusema walipata ushahidi wa mwingine juu ya mashtaka yaliyokuwa yakimkabili.
Mwezi Agasti 2024, rapa huyo alikubali na kukiri mashtaka hayo pamoja na ya kuhusishwa na mtandao unaodaiwa kuwa wa dawa za kulevya.
Leave a Reply