Yanga yaendeleza ubabe mbele ya Simba

Yanga yaendeleza ubabe mbele ya Simba

Klabu ya #Yanga wameendeleza ubabe kwenye ‘Derby’ ya pili ya msimu huu baada ya kuibuka na ushindi mwingine wa mabao 2-1 dhidi ya watani, #SimbaSc katika dimba la Benjamin Mkapa.

Yanga walipata mabao yote kipindi cha kwanza ambapo Aziz KI alifunga bao kwa mkwaju wa penalty  dakika ya 20 baada ya kufanyiwa faulo ndani ya boksi  na beki wa Simba  Husssein Kazi, bao la pili lilifungwa na JosephGuede dakika ya 38 na kipindi cha pili Simba waliweza kupata bao 1 lilifungwa na Freddy Kouablan  dakika ya 74.

Wananchi wanakwenda mpaka pointi 12 mbele ya mpinzani wao wakifikisha alama 58 baada ya ‘mechi’ 22 huku Wekundu wa Msimbazi wakisalia nafasi ya tatu alama 46 baada ya mechi 21.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags