Yammi uvumilivu umemshinda, Amkumbusha nandy majukumu yake

Yammi uvumilivu umemshinda, Amkumbusha nandy majukumu yake

Mwanamuziki wa #BongoFleva nchini #Yammi ambaye anafanya kazi chini ya lebo ya 'African Princess', ameonesha kuchoka kusubiri kutoa kazi mpya na kuamua kumkumbusha boss wake ambaye ni #Nandy ageukie upande wake.

Hayo yamekuja baada ya #Nandy ‘kupost’ kwenye ukurasa wake wa Instagram, mafanikio ya 'Dah remix', aliyowashirikisha wasanii wa Hip-hop #JohMakini, #Rosaree, #GNako, #Khaligraph, #Moni na #Stamina, huku akitaka kufanya remix na wasanii wa singeli.

Yammi aliijibu ‘posti’ hiyo kwa kuandika “kwa sasa inatosha sasa geukia upande wangu”.

Ikumbukwe kuwa Yammi mwezi uliopita alitoa wimbo uitwao ‘Love Crazy’ akiwa na wasanii #Lexsil na #ZiiBeats .
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags