Yamal Mchezaji Bora Chipukizi Euro 2024

Yamal Mchezaji Bora Chipukizi Euro 2024

Kiungo wa Klabu ya Barcelona na Timu ya Taifa ya Hispania, Lamine Yamal akiwa na mdogo wake baada ya kuchaguliwa kuwa Mchezaji Bora Chipukizi wa Michuano ya EURO 2024.

Yamal amekuwa Mchezaji Bora Chipukizi wa Michuano ya Euro 2024, huku akiweka rekodi ya mchezaji kijana zaidi kufunga bao katika mashindano hayo alipofunga hatua ya nusu fainali dhidi ya Ufaransa.

Nyota huyo alifunga bao hilo akiwa na miaka 16 na siku 362, akiipiku rekodi ya Johan Vonlanthen aliyefunga katika michuano hiyo mwaka 2004 akiwa na miaka 18 na siku 141.

Pia Yamal bao lake hilo limeweka rekodi ya kuwa mchezaji mdogo zaidi kufunga katika michuano ya timu za taifa kwa wakubwa akiipiku ile ya Pele alipofanya hivyo akiwa na miaka 17 na siku 239 kwenye michuano ya Kombe la Dunia 1958.

Aidha licha ya kusakata kabumbu kisawasawa huku akiwasumbua wakubwa uwanjani, umaarufu wa Yamal umeendelea kukua zaidi baada ya picha zilizopigwa mwaka 2007 kusambaa mitandaoni zikimuonesha akiwa mtoto mdogo wa miezi sita akiogeshwa na nyota wa soka, Lionel Messi.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Red Death

I design and develop services for customers of all sizes, specializing in creating stylish, modern websites, web services, Software's and online stores


Latest Post

Latest Tags