Yafahamu mashindano ya wanaume kubeba wake zao, Zawadi bia

Yafahamu mashindano ya wanaume kubeba wake zao, Zawadi bia

Inafahamika kuwa ulimwenguni kumekuwa na mashindano ya aina nyingi ambayo hufanyika kwa lengo la kuburudisha washindani na watazamaji. Wakati baadhi ya watu wakiwa wanaupenda mchezo wa mpira wa miguu huku wengine wakijipatia kipato kutokana na mchezo huo fahamu kuwa nchini Finland kuna mashindano ya wanaume kubeba wake zao huku mshindi hupewa zawadi ya bia yenye ujazo sawa na uzito wa mkewe.

Mashindano hayo yamekuwa yakipata washiriki kutoka maeneo mbalimbali ulimwenguni ambao wengi wao huwa wapenzi wa pombe, hufika nchini Finland kushiriki katika mashindano hayo ambayo huanza kwa mwanaume kubeba wake zao shingoni yake huku miguu ikining’inia chini na kisha kuanza kukimbia kwenye njia mbovu yenye mabonde,kwenye mchanga na kisha kwenye bwawa la maji na baada ya kotoka nje atakayekuwa wa kwanza ndiye huibuka mshindi.

Mshindano hayo huwa na sheria kwa mke hutakiwa kuwa na umri kuanzia miaka 17 na kilo kuanzia 49. Kawaida tamasha hilo hufanyika ndani ya siku mbili, na  kwa sasa limeanza kutambaa na maeneo mengine kama vile Uingereza, Marekani, Australia, India na Ujerumani.

Mashidano hayo yamekuwa yakifanyika kila mwaka mwezi Julai na yalianza tangu mwaka 1992 nchini Finland.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post