Wolper: P hagombezwi ndivyo alivyo

Wolper: P hagombezwi ndivyo alivyo

Muigizaji Jackline Wolper amewajibu mashabiki wanaodai kuwa mtoto wake wa kwanza #P pengine anagombezwa na dada wa kazi wa nyumbani, ndio maana mtoto huyo anaonekana kuwa muoga na asiye na furaha.

Maneno hayo ya mashabiki yamekuja ikiwa imepita siku moja tangu #Wolper a-post picha na video za watoto wake, huku sura ya mtoto huyo wa kwanza ikionekana kuwa tulivu kupitiliza na isiyo na furaha.

Katika majibu ya Wolper amedai kuwa mtoto huyo sio mpole kama watu wanavyo fikiria bali, ni kawaida ya kwao kwani hata baba yake pia ana sura ya upole.

Wolper amejibu kwa kuandika,
“haya sasa Ngoja niwajibu wote asanteni kwanza kwa upendo Asanteni kwa wishes na kila kitu ila kuhusu p kuwa mpole siyo kweli ila ndio walivyoumbwa yeye na baba yake ma pia baba yake mdogo ndio walivyo kwao wana sura ya upoke upole hakuna hapo kwanzia baba mtu hadi mtoto mtu😂😂ila niwastarab tuu mbele za wageni hapo kulikua na makameraman na Tupo ugenini ila ni Bingwa tuu ata wa kumdonoa kwa mbali dada yake 😂so msiseme anagombezwa weee hivi mnanijua mnanisikia kuna mmoja hapo kasema anagombezwa na dada wa kazi nataka tuu niwape habari kwamba mama ni askari mmoja ambaye ukicheza na hizi kazi mbili hapo umeumia yani siyo tuu kugombeza ata ukimkata jicho baya umekwenda na maji kwa hilo niwatoe wasiwasi kamanda nipo vzuri sanaa"

"Nawakumbusha ni mepushiii so uchungu wote nimepitia sitokua tayari anyanyasike nipo kuweni na amani kabisa..ukisoma vizuri utaelewa ukikurupuka ukachachawa utoelewa sinaga muda wakuremba maandishi kama sina ela😂😂haya majibu mmeridhika hee?? haya mwanzo na mwisho kusema anaonewa huyo king of My heart ok byeeee”






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags