Willow Smith: wanaamini nimepata mafanikio kupitia wazazi wangu

Willow Smith: wanaamini nimepata mafanikio kupitia wazazi wangu

Willow Smith ambaye ni mtoto wa mwigizaji kutoka nchini Marekani, Will Smith, ameweka wazi kuwa mafanikio aliyonayo hayatokani na wazazi wake bali ni juhudi zake mwenyewe.

Willow Smith wakati alipokuwa kwenye mahojiano na jarida la Allure, ameeleza kuwa watu wanafikiri sababu ya yeye kufanikiwa ni kutokana na wazazi wake jambo ambao siyo kweli kwani anaamini amepata mafanikio hayo kutokana na kupambania ndoto zake.

Aidha, aliongezea kwa kueleza kuwa hapo awali alitumia nguvu nyingi na bidii kujaribu kuwaonyesha wanaosema kuwa amepata mafanikio kupitia wazazi lakini sasa hatofanya hivyo tena ataacha kazi zake ziongee.

Willow Smith ni mwigizaji pamoja na mwimbaji anatamba na ngoma zake kama ‘Wait a Minute’, ‘Whip My Hair’, ‘alone’ huku akionekana katika filamu kama ‘I Am Legend’, ‘A Man Named Scott’, na nyinginezo






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags