Will Smith na Michael Jordan kuja na muendelezo wa i am legend 2

Will Smith na Michael Jordan kuja na muendelezo wa i am legend 2

Mwigizaji kutoka Marekani Will Smith ameweka wazi kuwa yeye na mwigizaji mwenziye Michael B. Jordan wanampango wa kutoa muendelezo wa filamu ya ‘I Am Legend 2’.

Smith ameyasema hayo wakati alipokuwa kwenye mahojiano na ‘Entertainment Tonight’ ambapo alieleza kuwa yeye na Jordan walikutana wiki kadhaa zilizopita na kila mmoja alikuwa na mawazo madhubuti kuhusu muendelezo wa filamu hiyo, hivyo basi anaamini filamu hiyo itakuwa ya kuvutia sana.

Ikumbukwe kuwa filamu ya asili ya ‘I Am Legend 2’ ilitokana na riwaya ya Richard Matheson (1954), ambapo Smith aliigiza kama mwanasayansi Robert Neville, mwathirika pekee katika ulimwengu aliyedhuriwa na viumbe wa ajabu (zombie).






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags