Will Smith na Martin Lawrence watoa ushauri kwa wapendanao

Will Smith na Martin Lawrence watoa ushauri kwa wapendanao

Baada ya kukutana na changamoto katika ndoa zao waigizaji Will Smith na Martin Lawrence, wametoa ushauri kwa wanandoa na wapenzi kwa kusisitiza kutendeana mema.

Wawili hao wameyasema hayo walipokuwa kwenye mahojiano na 'GOAT Talk' ambapo kwa upande wa Martin ambaye ndoa yake ya kwanza ilikuwa na Patricia Southall (1995-1997) na ya pili alifunga na Shamicka Gibbs (2010-2012), alitoa ushauri kwa kueleza kuwa wanandoa anatakiwa kutendeana mambo ya kupendeza.

Mwigizaji huyo wa ‘Bad Boys: Ride or Die,’ aliongeze kwa kusema kuwa talaka zake mbili zimekuwa zikimtesa.

“Nina talaka mbili ambazo zinanitesa sana siwezi kuzisahau kuna muda naboreka sana” amesema Martin Lawrence

Aidha kwa upande wa Will Smith ambaye mwanzoni alikuwa na Sheree Zampino na baadaye akazama Jada Pinkett Smith alishauri kuwa mtu awapo kwenye mahusiano anatakiwa kitimiza furaha binafsi kwanza unapokuwa kwenye mahusiano unatakiwa kutizama furaha yako kwanza.

“Haiwezekani kumfurahisha mtu, lazima ugundue furaha yako na kuifurahisha nafsi yako kwanza, ndiyo mje pamoja kushiriki furaha mliyonayo dhidi ya kujaribu kupata furaha wote”, amesema.

Utakumbuka kuwa Oktoba 2023 mke wa Will Smith, Jada Smith alitangaza kutengana kwa siri na mumewe huyo miaka saba iliyopita huku akidai kuwa wawili hao hawana mpango wa kupeana talaka.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags