Will Smith kukiwasha tuzo za Bet

Will Smith kukiwasha tuzo za Bet

Mwigizaji na ‘rapa’ wa Marekani Will Smith ameripotiwa kurudi tena jukwaani kama mwanamuziki ambapo anatajiwa kutumbuiza katika Tuzo za BET.

Katika taarifa iliyotolewa na BET ambayo haijaeleza kwa ndani majukumu ya Smith siku hiyo, lakini wameamua kumrudisha tena jukwaani mkali huyo wa ‘Bad Boys’ huku baadhi ya tetesi katika mitandao ya kijamii zikidai kuwa Will Smith anatarajia kuachia album mpya hivi karibuni.

Tuzo za BET zinatarajiwa kutolewa Juni 30, 2024 nchini Marekani huku mwanamuziki Usher akijipanga kupokea tuzo ya heshima ya ‘Lifetime Achivement’.

Will Smith kwa sasa anatamba na filamu yake ya ‘Bad Boys: Ride or Die’ iliyoachiwa Juni 7 mwaka huu, ambayo mpaka kufikia sasa imeingiza zaidi ya dola 289.2 million.

Mbali na kutoa filamu kali ambazo zimemuingizia maokoto ya kutosha amewahi kutamba na ngoma zake kama ‘Gettin' Jiggy Wit It’, ‘Just the Two of Us’, ‘Wild Wild West’ na nyinginezo kibao.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags