Whozu aonesha sura ya mtoto wake

Whozu aonesha sura ya mtoto wake

Unaambiwa bwana, kwa mara ya kwanza Msanii Whozu ameonesha sura ya mtoto wake aliyepewa jina la Lola ambaye yeye pamoja na Tunda wamebarikiwa kumpata mwaka 2021.

Sasa bwana!! kutoka kwenye ukurasa wa Instagram wa Whozu ametoa ya moyoni  na kueleza sababu za kumficha mwanaye ameandika hivi.

“LoLa Mrembo wangu Baba yako Nilikuficha sana Nilitaka ukue Vizuri ila Walimwengu bahati mbaya Wamenizidi nguvu
Na sisi Tumeshaamua Kumtegemea Mwenyezi Mungu tu. kila siku nikikubeba nakwambia Baby unatabasamu zuri sana. Umeamua Kunichukua mimi kidogo Umechanganya na Rangi Na lips za Mama yako Basi ndo Umekuwa Kacute zaidi.”

“Nikwambie tu Mwanangu, instagram ni maisha ya Teknolojia Utasifiwa, Utatukanwa pia, utaambiwa kila kitu Yani ilo wala lisikuumize kichwa kwanza sio shida zako Mwanangu Mimi Baba yako nipo Nyuma yako kwa lolote lile. Mungu Akulinde Endelea kukua TuEnjoy Mwanangu.”  Whozu

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm


Latest Post

Latest Tags