WHO yatoa tahadhari kuhusu dawa ya kikohozi ya maji

WHO yatoa tahadhari kuhusu dawa ya kikohozi ya maji

Shirika la Afya duniani (WHO) limesema kwamba shehena ya dawa ya kikohozi yenye sumu ya India  imepatikana katika visiwa vya Marshall na Micronesia.

WHO ilisema kuwa sampuli zilizofanyiwa vipimo vya dawa ya Guaifenesin TG syrup, iliyotengenezwa na kiwanda cha madawa cha Punjab QP Pharmachem Ltd, zinaonyesha kiwango kisichokubalika cha diethylene glycol na ethylene glycol.

Viungo vyote hivyo viwili ni sumu kwa binadamu na vinaweza kusababisha kifo iwapo mwanadamu atainywa. Taarifa ya WHO haikuelezea wazi iwapo kuna yeyote aliyeugua kutokana na matumizi ya dawa hiyo.

Tahadhari ya hivi karibuni inakuja miezi kadhaa baada ya WHO kuhusisha dawa nyingine za maji za kikohozi zilizotengenezwa nchini India ambazo zilisababisha vifo vya watoto katika nchi za Gambia na Uzbekistan.

Sudhir Pathak, ambaye ni Mkurugenzi mkuu wa QP Pharmachem, amewaambia baadhi ya vyombo vya habari kuwa kampuni ilikuwa imepeleka shehena ya chupa 18,346 katika mataifa ya Cambodia baada ya kupewa ruhusu ya kufanya hivyo. Alisema kuwa hakujua iwapo bidhaa hiyo ilikuwa imefika katika Visiwa vya Marshall na Micronesia.

Chanzo BBC

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags