WHO’S HOT: RODJAZZ

WHO’S HOT: RODJAZZ

RODJAZZ

Birthday: May 8th, 1996

Kazi: Musician

Rodjazz (Rodgers George) ni mwanamuziki wa Kitanzania anayefanya muziki wa maadhi ya Bongo Fleva, Afro Pop RnB, na Soul.

Amerekodi EP (extended playlist) ya Barua ya Mapenzi iliyoingia sokoni Februari 2022 akiwa chini ya lebo ya muziki, Bytes Music.

Ni mzaliwa kutoka Mwanza, mwaka 1996, Mei 8.

Rodjazz ana shahada ya mawasiliano ya umma kutoka Chuo Kikuu cha Tumaini, Dar es Salaam.

Kabla ya EP yake, Rodjazz amerekodi nyimbo jarada (cover songs) pamoja na kushiriki katika maandalizi ya wimbo wa "Nchi Yangu" ambapo ameimba pamoja na wasanii wengine akiwemo Jux Joel Lwaga, Nandy na Nikki wa Pili.

Ni chipukizi anayetamani kuwa nyota katika tasnia ya muziki na kuacha alama ya mabadiliko chanya kupitia kipaji chake. 

Rodjazz pia ni mtumbuizaji mwenye uwezo mkubwa wa sauti inayompa uhuru wa kuimba ‘live’ jukwaani na kukonga hisia za wapenzi wa muziki. 

Kipaji chake kilianza kujidhihirisha tangu akiwa mtoto wa miaka mitano alipoanza kuimba kwenye kwaya kanisani.

Rodjazz pia ni mwanahabari chini ya Nukta Tanzania.

 

Leo, Rodjazz anatupambia kipengele cha WHO’S HOT, kinachokujia kila IJUMAA katika jarida la Mwananchi Scoop. Don’t forget to check out his new EP on all digital platforms.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Detricia Pamba

A Digital Journalist, Content Creation Executive at Mwananchi Communications Ltd and Chief Editor of Mwananchi Scoop. I'm also writes stories around Technology, every Wednesday on Mwananchi Scoop. My other famous segments on Mwananchi Scoop include LISTI and WHO’S HOT.


Latest Post

Latest Tags