West Ham washindwa kumkatia tamaa Maguire

West Ham washindwa kumkatia tamaa Maguire

Inadaiwa ‘klabu’ ya #WestHam imerudi tena kwenye mazungumzo na ‘klabu’ ya  #ManchesterUnited ili kumchukua ‘beki’ wa kati wa ‘timu’ hiyo, Harry Maguire katika dirisha hili la usajili.

Aidha katika mazungumzo hayo, ‘timu’ ya West Ham imetoa ‘ofa’ kwa Man United kulipa kiasi kidogo cha pesa kwenye kile ambacho wanatakiwa kumlipa Maguire ili aondoke.

licha ya kuwa mchezaji huyo amebakisha miaka miwili kwenye mkataba wake wa sasa amedai kutaka kulipwa zaidi ya Pauni 7 milioni ili aondoke na West Ham ilifikia makubaliano ya kulipa Pauni 30 milioni na kumsajili Maguire kwa mkataba wa miaka 4 kisha kumlipa mshahara wa Pauni 120,000 kwa wiki ikiwa ni pungufu ya Pauni 70,000.

Ingawa beki huyo anataka pesa zaidi na kama itashindikana itabidi aendelee kusalia katika ‘timu’ yake ambako anaamini ndani ya miaka miwili iliyobakia atavuna pesa nyingi zaidi ya pesa ambayo ‘timu’ hiyo itamuza kwa sasa.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags