Wenner matatizoni kwa ubaguzi wa wasanii weusi na wanawake

Wenner matatizoni kwa ubaguzi wa wasanii weusi na wanawake

Jann Wenner ambaye ni mmoja ya waanzilishi wa Rock and Roll Hall of Fame Foundation na  mtayarishaji wa jarida la Rollind Stone afukuzwa kwenye ‘bodi’ ya Rock na Roll Hall of Fame Foundation kutokana na kutoa maneno yenye ubaguzi kwa wasanii weusi na wanawake.

Katika maneno yake Wenner amedai kuwa wanamuziki wenye ngozi nyeusi na wanawake si watu wa kuongea sana kama ilivyo kwa wazungu, kwani hawana uwezo mzuri wa utamshi wa maneno kama ilivyo kwa wazungu, huku akitolea mfano wasanii kama Stevie Wonder na Joni Mitchell.

Kutokana na kauli hiyo ilizua hasira na kupelekea watu kuiona ni kauli ya ubaguzi na ndipo ikapelekea kufukuzwa kwenye bodi ya Rock and Roll Hall of Fame, kwani wao wanasimamia usawa na hawakubaliani na ubaguzi wowote wa rangi wala kijisia.

Rock and Roll Hall of Fame Foundation inajihusisha na makumbusho ya utamaduni wa muziki wa rock na kumbukumbu za watu maarufu na ilianzashwa mwaka 1983.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post