Wema Sepetu hajarudia makosa

Wema Sepetu hajarudia makosa

Mwigizaji mkongwe na mfanyabiashara Wema Sepetu ni kama amejifunza kutokana na yaliyotokea mwaka 2023 katika kumbukizi ya siku ya kuzaliwa kwake, kwani mwaka huu amefanya sherehe ya siri na watu wake wa karibu.

Siku mbili zilizopita ilikuwa siku ya kumbukizi ya kuzaliwa kwa nyota huyo, akitimiza miaka 38, katika siku hiyo aliripotiwa kufanya sherehe na watu wake wa karibu jambo ambalo halijazoeleka.

Utakumbuka katika siku ya kuzaliwa ya mwigizaji huyo 2023, alifanya sherehe iliyohudhuriwa na mastaa wengi, lakini iliingia doa baada ya mama yake mzazi kutoa maneno ambayo hayakumpendeza Wema mbele ya wageni waalikwa.

Chanzo cha karibu cha mwigizaji huyo kiliiambia Mwananchi Scoop kuwa Wema alifanya sherehe ambayo alialika watu wake wa karibu akiwemo mpenzi wake Whozu, mwanamitindo Martin Kadinda, msanii Lulu Diva, Zuu 'Mama Steve' mzazi mwenzake Barnaba na wengine wachache.

Hii ni tofauti kwa Wema kwani amezoeleka kufanya sherehe kubwa na kuwaalika watu mbalimbali maarufu huku akijipongeza kwa zawadi zenye gharama ili kunogesha sherehe zake.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags